IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO KWA MAKAMANDA WA POLISI

0

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa. Katika mabadiliko hayo amemuhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pili Omary Mande ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Ruvuma kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marco Godfrey Chillya ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Konyo ambaye amestaafu.


Pia, amemhamisha aliyckuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gaudianus Felician Kamugisha, kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Haji Seti aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top