JELA MIAKA 70 KWA KUTOROSHA NA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 13

0

Mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imemhukumu mtu mmoja kwenda jela miaka 70 na kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa makosa ya kumtorosha binti mwenye umri wa miaka 13 na kumbaka.


Aliyehukumiwa ni Kulwa Meleka mkazi wa kijiji na kata ya Nkololo wilayani Bariadi na hukumu hiyo imetolewa na hakimu
mkazi mkuu wa mahakama hiyo Caroline Kikiwa baada ya kuridhishwa na maelezo ya upande wa mashtaka.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa serikali Vailet Mshumbusi aliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kuanzia Novemba mwaka jana hadi Marchi mwaka huu katika maeneo tofauti.
"Novemba 2021 alimtorosha mtoto huyo (jina linahifadhiwa ) kutoka kijiji cha Katente wilaya ya Bukombe mkoani Geita...tarehe tofauti tofauti kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 2021 alimbaka binti huyo akiwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma,"amesema na kuongeza,
"Desemba 2021 mpaka Marchi 10 ,2022 Mshitakiwa alimbaka mtoto huyo akiwa kijiji Mwasinasi wilayani Bariadi mkoani hapo...mshitakiwa ni mganga wa kienyeji ambapo alikuwa akimtishia binti huyo wakati anambaka kwamba akijaribu kushtaki kokote hatoweza kupata ujauzito" amesema Wakili Vailet .
Mshitakiwa kwenye utetezi wake aliiomba mahakama imsamehe ambapo wakili wa serikali Mushumbusi aliomba mshitakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye nia ya kutenda kosa kama hilo alilolitenda mshitakiwa na pia kulipa fidia kwa mhanga.
Hakimu Caroline Kiliwa alimhukumu mtuhumiwa kwa kosa la kwanza la kutorosha mtoto kutumikia kifungo cha miaka 10 jela , kosa la pili la kubaka alimhukumu kifungo cha miaka 30 jela ,kosa la tatu la kubaka kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top