Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kamishina wa msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha mbwa na farasi kimejipanga vyema kukabiliana na madawa ya kulevya Pamoja na vilipuzi vya aina yeyote ile katika mkoa wa Arusha.
Kamanda Masejo amesema hayo leo agosti 12 2022 wakati alipotembelea kikosi hicho kwa ajili ya kukagua mazoezi maalum ya mbwa ambao wanatumiwa na Jeshi la Polisi kuwatambua wahalifu mbalimbali wakiwemo wamadawa ya kulevya, silaha Pamoja na mabomu.
Sambamba na hilo kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo kupitia kikosi cha mbwa na farasi kinatoa mafunzo kwa mbwa wa kirai ilikuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Arushai.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha Mbwa na farasi mkoa wa Arusha mrakibu msaidizi wa Polisi ASP WILLIAM MWAISUMO amesema kuwa kikosi hicho kimejipanga vyema kutoa mafunzo kwa mbwa wote watao letwa kupata mafunzo ya ulinzi na utambuzi wa madawa vilipuzi.