Katika hali ya kushangaza mtoto mchanga amezikwa katika nyumba ya mtu aliyefahamika kwa jina la Furaha Nkwella iliyopo kata ya Mikoroshini wilayani Kyela.
Kwa mujibu wa mwenye nyumba hiyo Bi. Nkwella amesema amepata taarifa hiyo alipokuwa sokoni ndipo akapigiwa simu na mmoja wa wapangaji wake ambaye alikuwa akimwagilia mboga ya matembele kisha akabaini kuna kichanga kimezikwa katika eneo hilo mara baada ya kuona kiganja.
UMEISOMA HII;MABINTI WA DAMU CHAFU WAVAMIA KIJIJI...WENYE NDOA WAHAHA KUZINUSURU
Baadhi ya mashuhuda waliofika eneo la tukio wameshangazwa na kitendo hicho huku wakiwataka wanawake kutowatupa watoto badala yake kama hawawezi kuwalea ni vyema wakatumia njia za uzazi wa mpango.
Diwani wa kata hiyo Gwakisa George amesema tayari wametoa taarifa kwa jeshi la polisi na kuwataka baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuwa wavumilivu
Tutaendelea kukujuza kila hatua ambayo imechukuliwa.
Chanzo: Kyela fm