Mbunge wa Nzega Vijijini na Shabiki wa Simba Hamis Kigwangalla amesema suala la mjadala wa Bilioni 20 zilizoahidiwa na Mwekezaji Mo Dewji kwa Simba SC liko palepale lakini hiyo haimzuii kupongeza kuwa jezi mpya za Simba zilizooneshwa leo ni nzuri.
“Mjadala wa 20B uko pale pale lakini siwezi kupinga kila kitu hata wanavyopatia, mimi siyo ‘hater’ naheshimu na kushukuru juhudi na kazi nzuri, sinaga unafiki wa kusifia upuuzi…jezi hizi ni nzuri, kuna maeneo sikubaliani nao lakini nimeamua kunyamaza nisiharibu ladha”
Kwenye mfululizo wa tweets zake Kigwangalla aliandika “Jezi yetu kali sana kwa Watu wenye body zao unyama ni mwingi sana”
Hata hivyo mashabiki wengi wamejitokeza katika maduka ya Vunja bei kujipatia jezi za simba kabla ya siku ya Simba Day! agosti nane mwaka huu.
Una maoni gani kuhusu jezi za simba zilizozinduliwa leo? taundikie hapo chini nasi tutapata maoni yako!.