KIJANA AMUUA BABA YAKE KWA KOSA LA KUOA MKE WA PILI

0

 Polisi nchini Nigeria inamtafuta mtu mmoja wa makamo Kazeem Muhammed, baada ya kumuua baba yake na kukimbia kusikojulikana akimtuhumu kuoa mke wa pili.

Picha haihusiani na tukio halisi


Kazeem anadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji katika eneo la Kwankashe Suleja, Jimbo la Niger baada ya kukasirishwa na baba yake kwa kuoa mke wa pili zaidi ya mwaka mmoja uliopita akimtuhumu kuongeza ugumu wa maisha na kukosekana kwa furaha nyumbani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Trust, kaka wa marehemu, Isah amesema mara baada ya kutokea kwa mzozo huo Kazeem alimshambulia baba yake kisha kumuua na alikimbia na kwamba Polisi bado inaendelea na msako ili kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha Mahakamani.


Isah mesema, “Mvulana huyo ni mraibu wa dawa za kulevya na huwa anajihusisha na vitendo viovu na walipokuwa wakizozana asubuhi, alibeba ubao na kumpiga babaake ambaye alianguka sakafuni na alipogundua haamki alikimbia ndipo tukamuwahisha kaka yangu hospitali, lakini alifariki baadaye”.


Aidha alisema suala hilo limeripotiwa kwa mamlaka husika huku mabaki ya kaka yake yakiwa yamezikwa kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huku Polisi katika eneo hilo wakikataa kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa hawana mamlaka kwa mujibu wa Utaratibu.

TAZAMA VIDEO HII YA BABA ALIYEKAMATWA AKIMBAKA MTOTO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top