'KUBAKA KWA KIKUNDI' MWANAMME ASWEKWA RUMANDE MSICHANA ALIYEFANIKISHA UBAKAJI APEWA DHAMANA.

Hassan Msellem
0

Mahakama ya Mkoa Chake Chake juzi imempeleka Rumande Massoud Azizi Mohammed mwenye umri wa miaka 19 Mkaazi wa Pujini kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16.


Ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtka wa Serikali Seif Mohammed Khamis mbele ya hakimu wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji Muumin Ali Juma kuwa tarehe 22\07\2022 Majira ya saa 2 za Asubuhi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, msichana mwenye umri wa miaka 17 jina limehifadhiwa alimchukua msichana mwenye umri wa miaka 16 jina limehifadhiwa na kumpeleka kwenye Banda la Massoud Azizi Mohammed ambao alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji huku akijua kuwa kufanya hivyo ni Kosa kisheria.

Katika kesi hiyo msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 amejumuishwa katika shitaka hilo la kubaka kwa kikundi kwa kitendo cha kumchukua msichana huyo wa miaka 16 na kumpeleka kwenye Banda la Massoud Azizi Mohammed na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ingawa yeye amepewa dhamana kutokana na kuwa na umri wa chini ya miaka 18.

soma hii; MWANAFUNZI AUAWA NA MPENZIWE KWA KUKATAA KURUDIANA NAE

Kosa la kubaka kwa kikundi limeelezwa na sheria Nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar kifungu cha 108 (1) (2) (c) na kifungu Nambari 110 (1) (2) vya Sheria ya adhabu.

Kesi hiyo imepengwa kusikilizwa mashahidi tarehe 22\08\2022.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top