Madiwani watano Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoa wa Mtwara wamepigwa na butwaa baada ya kukuta barua zenye ujumbe zilizoandikwa kwa maandishi mekundu nyumbani kwao.
Jumbe zilizosomeka “Munatualibia maisha
yetu na nyinyi mujiandae kuhalibiwa kwa namna yoyote maisha yeny” jumbe hizo
zimendikwa kwa wino mwekundu huku mwishoni zikiwa na jina la diwani
aliyekusudiwa.
Jumbe hizo zimebandikwa katika nyumba
zao juzi usiku Agosti 2, 2022.
Akizungumzia ujumbe hiyo, Maya wa
Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile, alisema ameshangazwa na ujumbe huo
ambao mwishoni umeandikwa jina lake.
Amesema kila mmoja alikuta ujumbe
ukiwa kwenye bahasha umewekwa nyumbani kwake huku akisema jumbe hizo hazina
lengo zuri kwao kwa kuwa umelenga kuwatisha kwa jambo ambalo hawalijui.
“Sijui wanamaanisha nini ni ujumbe
huo yaani umekuwa wa vitisho kwangu sijui waliondika wanamaanisha nini na
kwanini walenge madiwani watano nikiwemo mimi” alisema
Alliendelea kusema “Niliupata
nilishtuka sana nilipowasiliana na baadhi ya madiwani nao wakawa na ujumbe ule
tulifika polisi kutoa taarifa ambao ni madiwani wa kata za Mtonya, Vigaeni,
Chuno, Naliendele na Ufukoni”
“Unajua Mtwara hatujafikia hatua hiyo
tuko salama na shughuli za maendeleo zinaendelea, sio utamaduni wetu kutishana
kama kuna watu ambao wamekwazwa na jambo watoe taarifa kwenye mamlaka husika
jambo hilo litafutiwe ufumbuzi sio sawa kutishiana na unaemtishia hajui nini kosa
lake” Shadida Ndile Meya Manispaa ya Mtwara Mikindani
Naye Diwani wa Vigaeni, Said Nassoro
alisema jambo hilo ni kubwa.
“Mimi sielewi kwanini wamefanya hivyo
kwa upande wangu sielewi kwanini mtu aseme kuwa tumemuharibia maisha na sisi
tujiandae kuharibiwa maisha yetu ni ujumbe mfupi lakini ni ujumbe ambao unazua
maswali mengi kwangu” alieleza
“Huu ujumbe aliona mwanangu
akanipigia simu kuna ujumbe na akapiga picha akanitumia nikashangaa kwanini
barua zinafanana na ndani ya bahasha kulikuwa na barua mbili yangu na Meya hii
ni kutishia amani ya mtu kama mtu kaweza kuja nyumbani kwako na kuweka ujumbe
huo anaweza kuja kufanya lolote” Said Nassoro
Mwananchi ilifanya jitihada za
kumpata kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nichodemus Katembo ambaye alisema
hana taarifa za barua hizo na atalifanyia kazi suala hilo.
Habari na Mwananchi.
Mwisho.