MAMA AMUUA MTOTO AKIDHANI NI NG'OMBE

0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Mwanamke mmoja aitwaye Estaroda Kaduma (28) amkazi wa Kichiwa kwa tuhuma za kumuua Mtoto wa Kaka yake anayefahamika kwa jina la Brown James Kaduma (7) ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kichiwa.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Kijana huyo alikuwa amelala majira ya saa nane usiku wakati Shangazi yake akiwa anafanya maombi lakini cha kushangaza alianza kupambana kwa kumpiga Mtoto akidhani ni ng’ombe mkubwa mweusi aliyefika wakati akifanya maombi.

“Huyu Dada huwa ana tabia ya kufanya maombi na katika maombi yake akaona ng’ombe mkubwa mweusi amefika katika eneo ambalo anafanya maombi, akaacha maombi akaanza kumpiga huyo ng’ombe na baadaye akatoweka baada ya muda akaonekana amefariki Kijana mdogo Mtoto wa Kaka yake baada ya kukanyagwakanyagwa kichwani na kujeruhiwa sehemu nyingine za mwili”

Kamanda Issah amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina na kutoa wito kwa Wananchi kuachana na imani hizo ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa kwenye jamii.
Baadhi ya wananchi wakishiriki ibada ya mazishi

Baadhi ya waombolezaji waktika katika shamba la Mungu kumsindikiza mrehemu kumhifadhi nyumba yake ya milele


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top