MARIDHIANO YA KISIASA NA USHIRIKIANO KATIKA JAMII NI MATUNDA YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA – MHE. OTHMAN

Hassan Msellem
0

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ni fursa muhimu kwa utekelezaji wa maridhiano ya kweli hapa visiwani, ili kuivusha Nchi kimaendeleo.


Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo, wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Marekani Nchini Tanzanzia Bw.Donald Wright, aliyefika Ofisini kwake Migombani jijini hapa, kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuhamasisha maendeleo kati ya Tanzania na Serikali ya Marekani.


Amesema kuwa GNU inaweka mazingira bora ya utekelezaji wa maridhiano ya kisiasa, sambamba na kuimarisha mshikamano wa kijamii, hali ambayo inatoa fursa ya kujenga demokrasia Nchini na kujiletea maendeleo, ambayo mara kadhaa kwa Zanzibar imekuwa ikikosekana.


Mheshimiwa Othman amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa ni sehemu muhimu katika utekelezaji wa dhamira ya kuleta umoja na maridhiano ya kitaifa, ambapo sasa hatua mbali mbali zimeanza kubainika, tangu Utawala wake, takriban mwaka mmoja uliopita.


Amebainisha utekelezaji wa dhamira hiyo kupitia hatua muhimu zikiwemo kuundwa kwa Kikosi-Kazi cha Kuratibu Mabadiliko ya Katiba, na pia Ziara ya hivi karibuni ya Mheshimiwa Rais Samia kisiwani Pemba, ambako jamii kubwa ni wahanga wa kisiasa hapa Nchini.


“Tunachoweza kubaini sasa ni dhamira ya utekelezaji wa mapendekezo ambayo yanatoa mwangaza wa kujenga mariadhiano na umoja wa kitaifa katika ngazi tofauti na hata kwa jamii”, ameeleza Mheshimiwa Othman.


Aidha amebainisha maeneo ambayo yanahitaji kujengewa uwezo ili kutekeleza maridhiano ya kisiasa, yakiwemo kukuza uelewa kwa umma, uwezeshaji wa mageuzi ya kisheria, kuimarisha hali ya kujiamini miongoni mwa raia, na kuhamasisha wadau wote juu ya umuhimu wa dhana ya amani na utulivu hapa Visiwani. 


Mheshimiwa Othman ametilia-mkazo utulivu wa kisiasa kama nyenzo na mazingira muhimu ya kujenga uchumi wa Nchi, huku akiahidi kwamba Zanzibar itaendelea kukuza mashirikiano ya muda mrefu na Serikali ya Marekani, kwa maslahi ya maendeleo ya pande zote mbili.


Naye, Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Bw. Donald Wright amepongeza juhudi hizo akisema kuwa ni hatua muhimu zinazoleta matumaini, na kuibua matarajio ya wananchi wa Unguja, Pemba na Tanzania kwa ujumla, katika kujiletea maendeleo.Ameeleza kuwa maridhiano ya kisiasa hapa Visiwani, ni fursa ya watu wote kuwa pamoja, kusahau tofauti za itikadi za vyama vyao, na kwamba Marekani haitowacha kuutumia mlango huo kuvutia wawekezaji na kuongeza fungu la misaada yake, ikiwemo ya kifedha kwaajili ya sekta mbali mbali zikiwemo za kuwapatia vijana ujuzi wa kitaalamu kupitia kilimo na ujasiriamali, ili kuungamkono mipango na miradi ya maendeleo.


Katika ujumbe wake, Balozi Wright aliambatana pia na Afisa Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Kristin Mencer.


Kitengo cha Habari.

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Agost 02, 2022.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top