Mchungaji wa Kanisa la KKKT Makedonia Lubaga Manispaa ya Shinyanga amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Shinyanga na kusomewa Shitaka la tuhuma za Kujaribu Kulawiti Mtoto wa Miaka 8.
Mchungaji huyo alifutiwa kesi ya awali namba 107, August 24 na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kwa sababu za Kisheria ambapo alikamatwa tena na kurejeshwa Mahabusu ambapo amekaa kwa muda wa siku 5 hadi hii leo alipofikishwa Mahakamani tena.
*Mtandaoni kuna #fursa nyingi sana*Je umewahi kujiuliza lile #bundle lako ambalo unijiunga kila siku au wiki na hata mwezi limekunufaisha vipi? Au ndo vile unaingia mtandaoni kusapoti ndoto na maono ya wengine🌝? Basi badili mtazamo wako Leo anza kutimiza ndoto zako LeoJisajili na fursa <<hapa>>>>
Akisomewa Shitaka hilo kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Marry Mrio Mshitakiwa huyo amekana shitaka linalomkabili la kujaribu kulawiti.
Mrio amesema kuwa Mshitakiwa huyo anatuhumiwa kutenda kosa hilo la kujaribu kulawiti mtoto wa miaka 8, August 12 eneo lilipo kanisa la Makedonia Lubaga kinyume na kifungu cha 155 cha kanuni ya adhabu, sheria namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.
Mwendesha Mashtaka upande wa Jamhuri Jukael Jairo amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekalimika na wako tayari kusoma hoja za awali na kusikiliza kesi hiyo.
Kwa upande wake wakili wa Utetezi Jeofrey Tuli ameiomba Mahakama hiyo Airisho kutokana na Mteja wake kutokuwa sawa kisaikolojia baada ya kukaa mahabusu kwa siku 5.
Wakili Tuli akaomba Mteja wake kupewa dhamana na hakimu alihoji upande wa Jamhuri ambapo umesema kuwa hauna kipingamizi na dhamana iko wazi.
Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Marry Mrio akamtaka mtuhumiwa kuwa na bondi ya milioni 3 pamoja na wadhamini wawili wenye kiasi hicho hicho cha pesa pamoja na mali isiyohamishika ambapo mmoja wa mashahidi amekidhi vigezo na mwingine kukosa vigezo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho ambapo mahakama hiyo itaanza kuwasikiliza mashahidi sita kutoka upande wa jamhuri na Mshitakiwa amepelekwa rumande.