Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikiria Mchungaji wa Kanisa la KKKT- Makedonia ya Lubaga Dayosisi ya Kusini Mashariki Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 8.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amewaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa August 12 baada ya jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kupokea malalamiko kutoka kwa moja ya familia za waumini wa kanisa hilo.
ACP Magomi amebainisha kuwa jeshi hilo linamshikilia mchungaji huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa ajili ya sababu za kiuchunguzi na kwamba uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Jeshi la Polisi hapa Shinyanga tunamshikilia Mchungaji wa Kanisa la KKKT kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka Nane majina yao tumeyahifadhi kwa ajili ya uchunguzi, na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”amesema Magomi