MJANE WA MREMA ASEMA AMEANZA KUPOKEA WATOTO WANAO DAI NI WA MREMA

0

 Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP Hayati Augustino Lyatonga Mrema, Doreen Mrema amesema kuwa hadi sasa ameshapokea watoto wa Hayati Mrema zaidi ya watatu (3) ambao walikuwa hawajatambulika kwenye Familia na ameahidi ataendelea kuwapokea na kuwalea kama mama yao na yupo Tayari kuendelea kuwapokea endapo tu ni kweli watakuwa ni watoto wa Mzee Mrema


Doreen amesema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari Mjini Moshi amabapo pia ametoa shukrani zake kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na watu binafsi kwa kuwa nao kipindi chote cha msiba.

"Alinieleza Nisiogope na niwapokee na niombe radhi kwenu, niwakumbatie na niwalee kama mama yao kama ambavyo yeye angewalea na ninamshukuru Mungu nimeendela kuwapokea watoto ambao walikuwa bado hawajambulika kwenye familia na sasa nimeshapokea zaidi ya watoto watatu (3). Mimi kama mama nitaendelea kuwapokea na kuwakumbatia kama ambavyo Mume wangu Mpenzi alivyoniasa siku 2 kabla ya kifo chake" - Mjane wa Mrema, Bi. Doreen Mrema.

Aidha amewahakikishia Watanzania kuwa ataendelea kumuenzi mume wake mpenzi (Hayati Mrema) na kuishi vile alivyomuasa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top