MKE AMFUKUZA MUMEWE NYUMBANI SABABU HANA KAZI ATAKA WAACHANE!

0

 Mwanamke mmoja nchini Marekani amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumfukuza Mumewe akitaka waachane na aende kuishi kwa Wazazi wake baada ya kushindwa kutafuta kazi na kumuachia bili zote alipe yeye bila ya usaidizi.Mwanamke huyo ameeleza kuwa Mume wake aliachishwa kazi muda wa miezi miwili iliyopita na amekuwa akiishi maisha ya starehe bila kujishughulisha kutafuta kazi nyingine.

Mnamo mwezi Juni, Mume wake alimwambia kwamba ameachishwa kazi na akadhani kwamba angeanza kutafuta kazi badala ya kupumzika na alipomuuliza juu ya kutafuta kazi nyingine, Mume wake alisema kwamba haoni manufaa ya kutafuta kazi nyingine.

"Nilianza kumlipia pesa za nje, nikimlipa pesa za safari za kutafuta kazi, wakati wote nikiwa na dhana kwamba angetafuta kazi mpya, lakini hakufanya hivyo, Mume wangu (32) na Mimi (30) tumeoana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, nina kazi nzuri na ninapata pesa nzuri lakini mume wangu amekuwa si Mtu wa kujishughulisha na kupata pesa nyingi kama Mimi”

Mara tu walipofunga ndoa, Mwanamke huyo alieleza kwamba Mume wake alipunguza saa zake za kazi bila kushauriana naye kwanza “Nimekuwa ni Mlezi mkuu, nikitengeneza pesa nyingi kwa ajili yetu sote ili afanye kazi za nyumbani kwa muda aliokuwa hana kazi, nimeendelea kulipa kodi na bili peke yangu huku yeye akitumia pesa kwa mambo mengine ambayo hatuwezi kuyahitaji kama Wanandoa”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top