Mchuuzi wa biashara ndogo ndogo mtaani mwenye ulemavu wa viungo raia wa Nigeria, Alika Ogorchukwu 39, amepigwa hadi kufa huku mashuhuda wakirekodi tukio hilo lililotokea kwenye barabara kuu ya maduka nchini Italia, bila kutoa msaada wowote.
Muitaliano wa Fillipo Ferlazzo 32, alimkaba
koo raia huyo wa Nigeria na kumsababishia kifo kwa kukosa hewa.
Mauwaji ya Ogorchukwu, yamewashitua
watu wengi wakiwemo raia wa nchi hiyo ya Italia, huku video za tukio hilo
zikisambaa kwa kasi mitandaoni na kuchapishwa katika tahariri za magazeti,
zilizozungumzia tukio hilo kwa kulihusisha na ubaguzi wa rangi.
Mbali na raia, wanasiasa wengi
wameoneshwa kuumizwa na tukio hilo ingawa kumeibuka kwa wasi wasi kuwa mauaji
hayo yanaweza kutumika kama kichocheo cha ubaguzi kabla ya uchaguzi wa kitaifa
nchini Italy September 2022.
Ogorchukwi, alikumbwa na mkasa huo baada ya kupeleka bidhaa zake kwa Muitaliano Fillipo Ferzallo na kisha kuondoka na baadaye Ferlazzo alimfuata kisha kuchukua fimbo yake ya kutembelea na kumpiga hadi kufa.
Shambulio linadaiwa kutokea eneo la
Civitanova Marche, mji wa pwani ya Adriatic, ambapo Februari 2018, mtetezi wa
mrengo wa kulia alipiga risasi na kuwajeruhi wahamiaji sita wa Kiafrika katiks
eneo la karibu la Macerata.
Miaka miwili kabla ya hapo, mwanamme
mmoja wa Nigeria pia aliuawa katika eneo la Fermo, ambako lipo upande wa kusini,
baada ya kujaribu kumtetea mke wake dhidi ya matusi ya kibaguzi.
Mama mzazi wa Alika Ogorchukwi, alilia kwa uchungu huku baadhi ya raia wa Italia wakimpa pole kwa kifo cha mwanae katika eneo