MTOTO AMUUA MAMA YAKE WA KAMBO KWA KUMKATA NA PANGA SHINYANGA

0

Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga linamshikilia kijana mwenye umri wa Miaka (20) Mikael Lubinza kwa tuhuma za kumuua mama yake wa kambo Mindesta Kadige (67) kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake huku chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa ni imani za kishirikina.


Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga ACP Leonard Nyandahu akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jumamosi tarehe 27/08/2022 majara ya saa 6 mchana huko kijiji cha Nyabubinza kata ya Lyamidati tarafa ya Nindo wilaya ya shinyanga mtuhumiwa alimvamia mama huyo na kumkatakata baadhi ya viungo vyake hadi kupelekea kifo kwa mama huyo.

"Mtuhumiwa alifika nyumbani hapo na kumkuta mama huyo akiwa sebuleni na kuanza kumshambulia kwa kumkata mapanga hadi kufa kwa madai mama huyo amekua akimroga na kushindwa kupata mafanikio kwenye maisha yake ndipo alipoamua kukatisha uhai wa mama huyo".

ACP Nyandahu amebainisha kuwa kwa sasa kijana huyo anashikiliwa na jeshi la polisi ambapo Upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kumuua kwa kumkata mapanga mama huyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top