MUME AMUUA MKEWE KWA KUMPIGA NA KITU KIZITO KICHWANI

0

 Mariam Masanja 22, mkazi wa Kijiji cha Nyabugela, Kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kung'atwa kidevu na mme wake Edward Franscis 20, ambao walikutana kwenye familia ya mwanamke kuhani msiba baada ya ugomvi wao wa muda mrefu.

Sehemu alipojeruhiwa marehemu


Wawili hao walikutana kwenye msiba wa kaka wa marehemu ambapo marehemu alikuwa mkoani Mwanza kwa dada yake baada ya kugombana na mme wake ndipo aliporudi kwao baada ya kusikia kaka yake amefariki.

Wazazi wa marehemu wameeleza walivyopata taarifa za mtoto wao kuuawa na mme wake huku baba mzazi wa marehemu anasema wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wa wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabugela Metusela Mgema, amesema wawili hao walifika mara kadhaa kwenye ofisi yake kwa ajili ya migogoro ndani ya familia yao ambayo ilikuwa inasuruhishwa mara kwa mara lakini mpaka kufikia kifo cha mwanamke wawili hao walikuwa wameachana.

Chanzo - EATV.

ULITAZAMA VIDEO HII YA KUTENGENEZA PESA ONLINE KAMA BADO USICHELEWE BOFYA SASA KUJIFUNZA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top