MUME AMUUA MKEWE SIKU CHACHE BAADA YA KUFUNGA NAE NDOA

0

 

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Msafiri Nasibu (31) mkazi wa kitongoji cha Maskati kata ya Tegetero Halmashauri ya Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Mariam Vitaris (19) na mtoto wake wa miaka 2 huku chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa ni mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitekeleza mauaji hayo usiku wa Agosti 10 mwaka huu ambapo mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa alienda kwa kaka yake Salum Said (34) ambaye anaishi katika kijiji hicho kwa lengo la kumuaga kuwa anasafiri na alipomhoji juu ya safari hiyo ndipo alipomueleza kuwa amefanya mauaji hayo nyumbani kwake ndipo kaka yake huyo aliamua kumkamata na kutoa taarifa Polisi.


Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu ambao ni wakazi wa kata ya Chamwino manispaa ya Morogoro wanaeleza kuwa mtoto wao alifunga ndoa na mume wake ambaye ni mtuhumiwa mwezi wa Julai mwaka huu na kuhamia kijijini huko na kwa kipindi chote hawakuwahi kusikia kama kuna mgogoro unaendelea mpaka kupata taarifa ya mauaji hayo. soma zaidi>>
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top