Mwalimu wa skuli ya msingi Madungu Chake Chake Pemba, alinayefahamika kwa jina la Ali Makame Hatib mwenye umri wa miaka 25, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasla la tano mwenye umri wa miaka kumi na moja (11) jina limehifadhiwa.
![]() |
Picha kutoka Maktaba. |
Akisimua chanzo kilimuwezesha
kugundua kwa mtoto wake kufanyiwa kitendo cha udhalilishaji, mama wa mwanafunzi
huyo alisema, siku ya Jummane ya tarehe 16, 2022 wakati mtoto wake akisikiliza kipindi cha
Kul-haku cha Radio Annour fm mtoto wake alisikia mada kuhusu udhalilishaji,
ndipo mtoto huyo aliporuka na kumuambia mama yake kuwa ameshadhalilisha na
mwalimu Ali Makam Hatib kwa siku kadhaa kutokana na vitendo alivyokuwa
anamfanyia
“Ilikuwa siku ya Jumanne ya tarehe
16, 2022 mwanangu akiwa anasikiliza kipindi cha Kul-haku kinachorushwa na Radio
Annour kulikuwa na mada kuhusu udhalilishaji akawa anasikiliza vile watangazaji
wanavyo zungumza kuhusu mada hiyo kisha kuruhusu watu kupiga simu na kuchangia
ndipo, mwanangu aliporuka na kuniambia mama kama ni hivyo mimi nimeshadhalilisha,
ni kamuuliza haya kundhalilishwa nani? Akinambia nimedhalilishwa na teacher
Ali, basi pale pale nikamuuliza haya teacher Ali kankudhalilisha vipi? Akaniambia
akaniambia hivi, kama teacher Ali alikuwa katika kunipiga alikuwa akinikunja
nguo na kunichezea sehemu zangu za siri napia alikuwa akinivua nguo sehemu
ambazo wanafunzo wangu hapo, baada ya hapo nikamchukua hatua ya kwenda Kituo
cha Polisi nilipofika polisi wakaniambia mkono kwa mkono nikaenda mkono kwa
mkono na kufanyia mahojiano na kisha kuchunguzwa na kuonekana ameshaharibiwa”
alisema mama mwanafunzi huyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini
Pemba kamishna msaidi za Polisi Abdalla Hussein Mussa, amethibitisha kumtia
mbaroni mwalimu huyo na kuahidi kufikishwa mahakamani pindi upalelezi utakapo
kamilika.
“Ni kweli tunamshikilia mwalimu wa
skuli ya msingi ya Madungu anayefahamika kwa jina la Ali Makame Hatib mwenye
umri wa miaka 25 akithumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa
miaka kumi na moja, tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12 mwezi wa 08 mwaka 2022
majira ya saa 11:30 za jioni huko maeneo ya skuli ya Mdungu ambapo alimuingilia
kimwili mwanafunzi huyo na atafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika,
wito wangu kwa wananchi kwamba tutii sheria bila ya shuruti na vile vile
tuwaache hawa wanafunzi wasome ili
baadae wawe ndoto nzuri maishani mwao” alisema
Inasemekana hili ni tukio la tatu la
ukabaji kufanywa na mtuhumiwa huyo.
Hadi idawaonline.com inatuma taarifa hii mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Madungu na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
kubakwa kwa mwanafunzi huyo wa darasa la tano (5) kuna timiza idadi ya wanafunzi nane (8) wa skuli ya msingi kubakwa kisiwani tangu kuanza kwa mwaka 2022 kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar.
Mwisho.