MWANAFUNZI ATUHUMIWA KUMUUA MWENZAKE KWA KUMPIGA NA TEKE

0

 Mtoto mwenye umri wa miaka (10), Jovina Simon ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Uwanja iliyopo kata ya Nyankumbu Mjini Geita amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na teke tumboni na mwanafunzi mwenzie Haruna Amin (16 )anayesoma darasa la saba katika shule ya msingi Mkombozi


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Ally Kitumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Leo Augusti 30,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema tukio hilo lilitokea Agosti 25, 2022 majira ya saa saba mchana katika mtaa wa elimu
Picha haihusiana na tukio halisi la mauaji-kutoka Maktaba

Kamanda Kitumbo amesema tukio lilitokea wakati Jovina na Haruna walipokutana na kulitolea ugomvi kati yao ndipo Haruna alipompiga teke tumboni na kusababubisha Jovina kupata maumivu makali na baadaye kukimbizwa hospitali.


"Alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita, hiyo Augusti 25 ambapo ilifika majira ya saa kumi na jioni Augusti 29,2022 alifariki dunia". Amesema Kitumbo

Kamanda Kitumbo amesema mpaka sasa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya Uchunguzi zaidi na Mtuhumiwa wa tukio hilo anashikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi ulikamilika taratibu za kisheria zitafuata

Wasafi media imefika nyumbani kwa Jovina Mtaa wa Elimu kata ya Nyankumbu mjini Geita na kuzungumza na baba mzazi wa Jovina anayefahamika kwa jina la Saimon John ambaye amesema siku ya tukio hakuwepo nyumbani alipigiwa simu na mkewe kuwa mwanae (Jovina) ameumia kwa kupigwa na mtoto mwenzie ambaye ni mtoto wa jirani.

"Nilirudi nyumbani baada ya mke wangu kunipa taarifa hiyo nikawakuta wako hospitali tayari alipatiwa matibabu siku ya kwanza ,ya pili na Augusti 29, 2022 alifariki'. Amesema Simoni

"Sijajua chanzo Cha ugomvi wao ila huyo mtoto ni jirani yangu wa chumba Cha pili, kipindi namuuguza hospitalini alisema mwenzie alimpiga na teke na ngumi chini ya ubavu"

"Baada ya kupima vipimo vya x- ray daktari alituambia amepigwa sehemu mbaya na bandama imeharibika vibaya na ndicho kilichopelekea kifo chake.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top