MWANAFUNZI AUAWA NA MPENZIWE KWA KUKATAA KURUDIANA NAE

0

Mwanafunzi wa kike wa chuo kikuu nchini Dubai ameuawa kwa kuchomwa kisu na aliyekuwa mpenzi wake kwenye mlango wa jengo karibu na Mahakama ya Jinai ya Zagazig siku ya Jumanne, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.



 Salma Bahgat mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa Kitivo cha Habari katika Chuo cha Al Shorouk, alichomwa kisu mara 15 na mwenzake Islam Mohammad Fathi mchana kweupe ambaye awali walikuwa wapenzi. 

Umeisoma hii:MABINTI WA DAMU CHAFU WAVAMIA KIJIJI...WENYE NDOA WAHAHA KUZINUSURU

Eneo la Zagazig ilitikiswa na mauaji ya kikatili ya Salma kwenye barabara yenye shughuli nyingi mbele ya mamia ya mashuhuda, kwa namna ile ile ya mauaji ya kutisha ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mansoura Naira Ashraf yaliyotokea mwezi juni mwaka 2022. 

Video ya mauaji ya Salma ilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, na kuzua malalamiko nchi nzima wakitaka kukomesha kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake hasa wanafunzi kuuawa kisa mapenzi. 

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, mshukiwa alimpiga mwathiriwa na kumwacha kwenye dimbwi la damu,baadaye alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi. 

Inaaminika kuwa mshukiwa alimuua Salma kwa kulipiza kisasi baada ya kuachana naye siku chache zilizopita.

Usisahau kushare habari kwa wengine na kutuachia maoni hapo chini.

Chanzo: Gulf News

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top