BABA WA MIAKA 50 AHUKUMIWA KWENDA CHUO CHA MAFUNZO (JELA) MIAKA 20 KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA SABA.
Mahakama maalumu ya makosa ya
udhailishaji Chake Chake, imemuhukumu kutumikia chuo cha mafunzo (Jela) kwa
muda wa miaka ishirini (20), Suleiman Rashid Juma almaarufu kwa jina King
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, mkaazi wa Pujini kwa kosa la kumlawiti
mvulana wa miaka saba.
Hukumu hiyo, imetolewa juzi tarehe
22\08\2022 na hakimu wa mahakama maalumu ya makosa ya udhalilishaji Muumini Ali
Juma.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na
mwendesha mashtaka wa Serikali Ali Amour Makame, kuwa siku tarehe 25\03\2022
majira ya saa 5 za asubuhi huko Pujini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini
Pemba, mtuhumiwa alimlawiti mtoto wa kiume wa miaka saba Jambo ambalo ni kosa
kisheria kwa sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar kifungu cha
sheria nambari 115(1).
Idadi ya mashahidi sita (6) ikiwemo
mtoto mwenyewe ambaye ni muathirika wa kitendo hicho, mwanafunzi wa darasa la
kwanza anayesoma darasa moja na muathirika, Baba Mzazi wa muathirika, Askari
mpelelezi, Daktari dhamana wa hospitali ya Chake Chake na Mkaguzi msaidizi wa
jeshi la Polisi shehia ya Pujini Kunvini, ushahidi ambao ulitosha kumtia
hatiani mshitakiwa.
Akisoma hokum hiyo, hakimu wa
mahakama ya makosa ya udhalilishaji Chake Chake Muumini Ali Juma, amesema kwavile
mshitakiwa hilo ni kosa lake la kwanza pamoja na kuzingatia ombi la mshitakiwa
kutokana na umri wake na hali yake, hivyo mahakama hiyo imezingatia kifungu cha
299 cha sheria katika utoaji wa adhabu wa kosa hilo pamoja na kifungu cha 314
cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sheria ya Zanzibar, sheria nambari
saba (7) ya mwaka 2018 kwa mujibu wa kifungu cha 115 (1) sheria nambari sita
(60 ya mwaka 2018 Sheria ya adhabu ya makosa
ya jinai, ambapo kosa hilo adhabu ya kifungo cha maisha lakini kwa
kuzingatia ombi la mshitakiwa amepewa adhabu ya kutumikia chuo cha mafunzo kwa
muda wa miaka ishirini pamoja na kulipa fidia ya shilingi milioni moja kwa
muathirika.
Ikumbukwe kuwa, tarehe 29\03\2022 kipindi
cha Mawio kiliripoti juu ya mshitakiwa huyo kushikiliwa katika kituo cha polisi
Madungu kutokana na tuhuma za kumlawiti mvulana huyo, ambapo kwa mara ya kwanza
mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani na mnamo tarehe 06\04\2022 dhidi ya
shitaka hilo.
Haki ya rufaa imetolewa kwa upande usioridhishwa na hukumu hiyo.
Mwisho.