PEPO LA KIFO LA WAANDAMA WANAFUNZI,MWINGINE TENA AJINYONGA NJOMBE

0

 Mwanafunzi wa darasa la sita, Marko Sanga (12) Mkazi wa Kijiji cha Maleutsi Wilaya ya Makete Mkoani Njombe amekutwa amejinyonga kwa madai kuwa ni kutokana na redio, nguo za shule pamoja na madaftari yake kuungua kwa shoti ya umeme.

RPC NJOMBE-Hamis Issa
Mama mkubwa wa Mwanafunzi huyo, Obina Mbilinyi amesema Mtoto huyo walikuwa nae shambani na jioni ilipofika walimwambia atangulie nyumbani ili akafungue ng'ombe malishoni na kuwarudisha nyumbani ambapo alipofika nyumbani alikuta vitu hivyo vimeungua kwa shoti ya umeme iliyosabishwa na radio ambayo Mwanafunzi huyo alikuwa ameichomeka kwenye umeme .

Amesema Marko alifungua ng’ombe kama alivyoagizwa na kisha akaenda kujinyonga “Tuliporudi nyumbani tulimtafuta na kumkuta akiwa amefariki huku akining'inia kwenye mnyororo wa baiskeli tunahisi kuungua kwa radio na baadhi ya vitu vyake inaweza kuwa ni sababu ya kujinyonga kwake maana mpaka tunaagana shambani alikuwa katika hali ya kawaida"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka Wazazi kuishi vizuri na Watoto wao kwani inawezekana Mtoto huyo alikuwa anahofia kuadhibiwa kwa kile kilichotokea ndipo akaona ni heri kufariki
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top