Rais wa Marekani Joe Biden amehutubia taifa la Marekani na kutoa kauli nzito juu ya kifo cha kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman Al-Zawahiri, aliyeuawa na ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani.
Rais Biden, amesema kuwa kifo cha Al-Zawahiri ni malipo ya unyama alioufanya
kwa wananchi wa Marekani kufuatia kuhusika katika utekelezaji wa shambulio la kigaidi
la September 11 mwaka 2001 ambalo liliua zaidi ya raia 3000 nchini humo.
Aidha kiongozi huyo wa kundi la
kigaidi ambaye ana asili ya Misri aliuawa majira ya asubuhi wakati akiwa katika
nyumba yake kwenye mji wa Kabul ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Rais Biden ni kwamba hakuna mtu mwengine yetote Yule kutoka katika familia ya
Al-Zawahiri ayeathirika au kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Al-Zawahiri aliuawa vipi?
Maafisa wa Marekani wanasema Zawahiri
alikuwa anasimama kwenye veranda ya nyumba yake ya mafichoni. Ghafla, Ndege
asiyokuwa na rubani, inayofahamika kama drone- ilidondosha makombora mawili.
Taarifa inasema kuwa kombora
lilimpiga Zawahiri ambaye alikuwa amesimama nyumbani kwake.
Ndugu wengine wa familia ya Ayman
Al-Zawahiri walikuwepo pamoja naye katika eneo hilo, lakini hakuna mtu mwengine
aliyeuawa wala kujeruhiwa katika shambulio hilo, na kiongozi wa AL-Qaeda akafa
mara moja pale pale peke yake, Maafisa walisema