SENEDA: WATUMISHI TUSITENGENEZEANE AJALI KAZINI TUPENDANE

0

 

SONGWE: Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka watumishi wa Mkoa wa Songwe kufanya kazi kwa kupendana, kuheshimiana na kuthamini kazi ya mwenzake ili kufanikisha malengo ya Taasisi.

Katibu Tawala, Bi. Happiness Seneda amesema hayo alipokutana na watumishi wa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa lengo la kufahamiana na kuweka mikakati ya kazi ili kufanikisha malengo ya Taasisi.

Bi. Happiness Seneda amewataka watumishi kutotengenezeana ajali kazini Ili mwenzako aweze kuaribikiwa na kazi, badala yake amewataka watumishi kukumbushana pale unapoona mwenzako anaenda kuaribikiwa basi una mwambia ili aondokane ha hali hiyo.

"Ndugu zangu watumishi tunategemeana kwenye kazi izi, ofisini bila katibu mhutasi ofisi haiendi, bila muhudumu ofisi haiendi hivyo kila moja aweze kuthamini kazi ya mwenzake" Bi. Happiness Seneda Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

Pia, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka watumishi kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo kujiendeleza kiuchumi wao na familia zao.

Amesema Mtumishi ulipo hapo ndio kuna fursa zitumie, kwani ukienda sehemu au ukiwa unaishi hapo ndio malaika wako wa Baraka walipo.

Wakati huo huo, Bi. Happiness Seneda amewataka watumishi kila mmoja kwenye nafasi yake kuwajibika kwa kufanya kazi ili kufikia malengo ya Serikali kwani Serikali inawategemea sana watumishi kufikia malengo ya kuwatumikia wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top