Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (mwenye kofia) akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku moja ya umuhimu wa chanjo ya Uviko 19 na wajibu wa waandishi wa habari



**********************
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amehaidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na waandishi wa habari kwa lengo la kuuletea maendeleo Mkoa huo.
Ameyasema hayo leo Alhamisi Agositi 18,2022 wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya umuhimu wa chanjo ya Uviko 19 na wajibu wa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kwa kwakushirikiana na taasisi ya kimataifa ya Internews.
UMEISOMA HII;TANO APELEKWA JELA MIAKA 30 SABABU YA BANGI!
“Binafsi nawapenda sana waandishi wa habari tangu niko Mara nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu sana waandishi wa habari,nimekwenda Tanga vilevile nimeshirikiana nao na sasa niko Mwanza naombeni tufafanye kazi kwakushirikiana kwa manuufaa ya Mkoa wetu na Taifa kwaujumla”,amesema Malima
Malima amewaasa wanahabari kuendelea kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo kuchanja ili kuweza kujikinga na kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema mafunzo hayo yawe chachu kwa waandishi kwa kuendelea kuihabarisha jamii juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
“Tumieni kalamu zenu vizuri katika kutoa elimu kwa jamii ili waelewe athali mbalimbali zinazoweza kujitokeza endapo watapuuza maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko Uviko 19”,amesema Malima
Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) Edwin Soko,amesema kampeni dhidi ya chanjo ya Uviko 19 imekuwa ni endelevu kwa klabu hiyo kwani wamekuwa wakifanya mafunzo mara kwa mara kwa waandishi wa habari kwaajili ya kuwapa uchechemuzi wa umuhimu wa chanjo ya Uviko 19 na umuhimu wa kuandika habari zinazolenga watu kujitokeza kupata chanjo hiyo.
Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa, amesema kuwa muitikio wa watu kuchanja ni mkubwa kwani hadi sasa Mkoa huo umefikia asilimia 76 ambayo ni lengo la kitaifa.