Vijana Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba wametakiwa kujitambua kwa kua mstari wa mbele kuendelea kutunza amani iliyopo katika jamii.
Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi Salum Omar Ussa kwa niyaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkani wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa makundi tofauti ya vijana wa wilaya hiyo.
Amesema vijana walio wengi wanafanya mambo kwa sindikizo na maslahi ya baadhi ya watu bila kutambua kwa wao ndio muhimili mkubwa wa utunzaji wa amani katika jamii zao.
Aidha amesema waathirika wakubwa yanapo tokea machafuko ya uvunjifu wa amani ni watoto, walemavu, anawake na wazee na hali hiyo inatokana na ukosefu wa njia sahihi ya utatuzi wa migogoro.
Awali akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya ZYCO Haroub Mmanga amesema mafunzo hayo yatawapa uweledi mzuri vijana katika kutafuta njia mzuri za utunzaji wa amani.
Kwa upande wake mjumbe kutoka foundation for Civil Society Jojina Lundi amesema mafunzo hayo yaliyo washirikisha vijana yanalengo la kufawafunza njia sahihi za utatuzi wa mogogoro na kuwakumbusha wajibu wao wa kutunza amani.
Akiwasilisha mada ya kwanza ya njia mabadala ya usuluhishi wa migogoro Moh'd Hassan Abdalla kutoka Jumuiya ya wasaidizi wa sheria chake chake, ametaja baadhi ya vyanzo vikubwa vya migogoro ni pamoja ukosefu wa elimu kuhusu suala lenye mgogoro, kutokuaminiana, na rushwa katika jamii.
Akiwasilisha mada ya haki na wajibu wa raia Mkurugenzi wa Juimuiya ya wasaidizi wa sheria Wilaya ya Mkoani Maalim Nassor Hakim Haji amesema, katika utunzaji wa amani katiba zote mbili ya Zanzibar na ya Tanzania zinaeleza haki ya uhuru na uswa kwa kila mtu pamoja na kuthaminiwa utu wake ili kuepusha migogoro katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku mbili yenye kengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kutunza amani na utatuzi wa nigogoro yameandaliwa na taasisi Zanzibar Youth Care Organization (ZYCO) kwa ufadhili mkubwa wa Foundation for Civil Society.