UKATILI; WANANCHI WAMZIKA MZEE AKIWA HAI ATUHUMIWA KWA USHIRIKINA!

0

Mzee Jonas Komba (78) Mkazi wa kijiji cha Mahanje Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma amezikwa akiwa hai na Wananchi wenye hasira kali kwa kushirikiana na baadhi ya Wanafamilia kutokana na tuhuma za kumuua Mtoto wake Severen Komba (34) aliyekutwa amefariki ndani ya nyumba yake.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema jambo hilo ni la kinyama kwa kuwa Wananchi wamejichukulia sheria mkononi kwa kumzika Mzee huyo akiwa hai badala ya mwili wa Mtoto huyo ambaye tayari alikutwa amefariki asubuhi bila ya kujulikana sababu za kifo chake, Mzee huyo amepoteza maisha baada ya kuzikwa akiwa hai.


“Walipofika hapa kwenye kaburi wakamuweka huyu Baba akiwa hai na kumfukia, hili ni jambo la kinyama sana,huu unyama hauwezi kuvumiliwa, hii tabia hatuwezi kuivumilia lakini jambo la kushangaza Vijana wake ndio wameongoza mashambulizi ya kumpiga Baba yao na kuja kumsimika ndani ya kaburi la marehemu Mtoto wake na kumfukia”

Picha kutoka Maktaba!


Mgema amesema Serikali haitaweza kuvumilia jambo hilo na tayari vijana wawili wa Familia ya Mzee huyo wamekwishakamatwa kwa kuongoza kumzika Baba yao akiwa hai huku wakiendelea kuwatafuta popote walipo Wananchi wengine waliotajwa kushiriki katika tukio hilo la mauaji na kuwachukulia sheria.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema Kijana Severin Komba alikutwa amefariki Agosti 12 majira ya saa nne asubuhi mara baada ya Wananchi kuvunja mlango wa nyumba yake kutokana na kutoonekana kwa muda mrefu huku mzazi wake akishindwa kwenda kushiriki katika mazishi na tayari alikuwa akituhumiwa kuwa Mshirikina kwa muda mrefu. soma zaidi>>

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top