Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mtoto mchanga amekutwa ametupwa katika jalala la taka katika soko la Kalumbulu wilayani Kyela asubuhi ya tarehe 7.8.2022.
Kichanga icho kilionekana mara baada ya watoto waliokuwa wakiokota vyuma jalalani kukiona na kupiga ukunga kuwataarifu watu walio karibu na jalala hilo.
kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni wafanyabiashara wa soko la Kalumbulu wamekadiria umri wa kichanga icho kuwa kati ya wiki zisizozidi mbili
Aidha wafanyabiashara hao wameonyesha kutofurahishwa na kitendo icho cha kikatili ambacho kimekuwa na muendelezo sehemu mbalimbali wakiwasihi wanawake ambao wanatupa watoto kutofanya hivyo kwani ni kosa kisheria pia watu wengi wamekuwa wakipambana kupata watoto.
Tunafanya juhudi za kuzungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya tutaendelea kukujuza kila linaloendelea