UNYAMA! MWANAMKE ALAWITIWA KISHA KUUAWA NA WASIOJULIKANA

0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limesema linachunguza kuuawa kwa Fatma  Bakari Suleiman  ambapo majira ya saa 12 kata ya mkuti aligundulika kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kulawitiwa kwenye gofu jirani na nyumbani kwao.


 Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi, Agosti 11, 2022 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemas Katembo amesema  mwili wake ulifanyiwa uchuguzi na kubaini chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa baada ya uso kugandamizwa ardhini kwa muda mrefu.

UMESOMA HII:WAFANYAKAZI PRIDE FM WADAI MISHAHARA MIEZI 26,

“Kwenye eneo la tukio vilikutwa kitambulisho cha mpiga kura, laini mbili za simu na kofia ambazo zitasaidia kwenye uchunguzi na zitatumika kama vielelezo,” amesema

“Lakini majira ya saa tatu usiku, marehemu akiwa na dada yake waliingia kula chakula cha usiku na haijulikani alitoka saa ngapi ndani hadi asubuhi walipobaini amefariki dunia jirani na nyumbani kwao,” amesema

Kamanda huyo amesema, “watuhumiwa wamekamatwa na wameshafikishwa mahakamani kasoro kesi moja ambayo mtuhumiwa bado hajapatikana.” 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top