WADAU NJOMBE WATAKIWA KUSHIRIKI KUHAMASISHA WATOTO KUPATA CHANJO YA POLIO

0

 Viongozi wa dini,waganga wa tiba asili na viongozi wa serikali za mitaa wametakiwa kushirikiana na watalaam wa afya kuhakikisha kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa polio inawafikia watoto wote waliopo chini ya umri wa miaka mitano katika halmashauri ya mji wa Makambako.


Wito huo umetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika kikao cha kamati ya afya msingi juu ya utekelezaji wa kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo wa polio,ambapo amesema ushirikiano baina ya taasisi za kidini,waganga wa tiba asili na wadau wengine utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kampeni hiyo ambayo itaanza septemba mosi mwaka huu.

Aidha katibu tawala huyo amesema licha ya hamasa kubwa kutolewa kwenye kampeni ya chanjo ya polio,kamati hiyo inatakiwa kuendelea kuhamasisha jamii kuendelea kujinga na magonjwa kwa kupatiwa chanjo ambazo zinatolewa na serikali.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa makambako na Hanana Mfikwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Keneth Haule wamesema wanauhakika kampeni hiyo itatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kuomba jamii kutambua umhimu wa chanjo hiyo ili kuwanusuru watoto na ulemavu wakudumu pamoja na kifo.

Naye Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Alexnder Mchone amesema chanjo hiyo itatolewa kwa awamu nne na nia ya serikali ni kuhakikisha ikabiliana na athari ambazo zinaweza kuwakuta watoto na ugonjwa wa polio ambao unasababisha kifo na ulemavu wa kudumu.

Baadhi ya wadau katika kikao hicho akiwemo mwenyekiti wa waganga wa jadi katika halmashauri ya mji wa Makambako Sijaona Mhadze na Hitra msola katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi wamesema watahakikisha jamii inapatiwa elimu sahihi dhidi ya chanji hiyo ya polio.

Halmashauri ya mji wa Makambako imetajwa kuongoza kimkoa katika utoaji wa chanjo ya polio ambapo imewafikia watoto asilimia 144 kwa awamu ya kwanza na asilimia 125 kwa awamu ya pili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top