WAFANYAKAZI PRIDE FM WADAI MISHAHARA MIEZI 26,WAOMBA SERIKALI IWASAIDIE

0

 Wafanyakazi wa Kituo cha Redio cha Pride FM,  wameiomba serikali kuwasaidia kupata stahiki zao zaidi ya Sh milioni 100 fedha ambazo ni mishahara ya miezi 26.

Hayo yamebainishwa leo na wafanyakazi hao, walipokuwa wakitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kwa lengo la kuiomba serikali, ili iweze kuangalia suala la haki zao wafanyakazi hao 22.

Wafanyakazi Pride FM wadai mishahara miezi 26

Akizungumza katika mkutano huo, Sospeter Magumba, amesema kuwa  taratibu mbalimbali zimefanyika kuhakikisha wanapata stahiki zao hizo ikiwemo kuzungumza na waajiri wao, Ramadhani Lutambi na Hamza Napunda, lakini hawakufanikiwa kulipwa.

UMESOMA HII KUTOKA MAGAZETINI LEO NI AGOSTI 12,2022 SOMA KURASA ZA MBELE NA NYUMA

Amesema pia wamezungumza na Idara ya kazi, Uongozi wa Mkoa, jitihada ambazo hazikuzaa matunda na athari za kukaa muda mrefu bila kupata stahiki zao zimekuwa ni kubwa kwao na familia kwa ujumla.

"Kuna baadhi yetu hapa imefiia hatua ya kutengana na familia zao, wengine kufukuzwa kwenye nyumba za kupanga kutokana na kushindwa kulipa kodi na sisi ni watu wazima tuna familia, ambazo zinatutegemea.

“Sasa inapotokea mazingira kama haya waajiri wetu kushindwa kutulipa mishahara yetu kwa kipindi chote hiki cha miezi 26, hii siyo haki na ukiukwaji wa sharia," amesema Magumba na kuongeza:

"Ombi letu kwa Serikali itusimamie katika hili ili hawa waajiri wetu watulipe hizi fedha zetu na sisi ni wanahabari, ambao tumechangia kwa sehemu kubwa maendeleo ya Mkoa  wa Mtwara na Taifa kwa ujumla, bado tuna ndoto za kuendelea kulitumikia Taifa letu," amesema.

Nae Andrew Mtuli ameiomba Wizara ya Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari,  kuliangalia suala hilo kwa macho mawili, kwani sasa hivi  siyo muda wa kuendelea kusubiri badala yake wapatiwe stahiki zao, ili kila mtu aangalie maisha mengine.

Kwa upande wake Meneja wa kituo hicho, ambaye pia ni miongoni mwa wafanyakazi hao wanaodai stahiki hizo, Justine Mshuza, amekiri kuwepo kwa madai hayo na kueleza kuwa hali hiyo imetokana na ugumu wa biashara,  hivyo kusababisha kuwepo kwa malimbikizo hayo.

Hata hivyo amesema jitihada zilizopo kwa sasa ni kwamba wamiliki wa Kituo hicho wameamua kuuza maeneo yao, ikiwemo eneo hilo ilipo redio, lakini pia wanaiuza na redio yenyewe, ingawa bado hawajapata wateja.

Chanzo; Habari leo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top