WANAFUNZI 19 WA KIDATO CHA KWANZA WALIOFAULU MICHEPUO 2021, KUTOKA SKULI NNE ZA JIMBO LA CHAMBANI WAZAWADIWA MIKOBA NA VIONGOZI WA JIMBO HILO.
Wanafunzi kumi na tisa (19) kutoka
skuli nne za jimbo la Chambani waliofaulu darasa la sita mwaka 2021, wameombwa
kuzidisha juhudi katika masomo ili kuendelea kufanya vizuri katika mitihani yao
ya kidato cha nne.
Mapema akikabidhi zawadi ya mikoba
kwa wanafunzi hao, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Wilaya ya Mkaoni Ndugu
Ali Juma Omar, amesema viongozi wa jimbo hilo wana nia ya dhati ya kuwaisadia
sekta ya elimu, hivyo basi amewaomba wanafunzi hao kuzidisha juhudi ili
kuendelea kufanya vyema katika masomo yao.
“Ndugu wanafunzi naomba
niwahakikishie kuwa viongozi wa jimbo hili ambao ni Mheshimiwa Mbunge,
mwakilishi pamoja madiwani wana nia ya dhati na kweli ya kuwasaidia wanafunzi
wa jimbo hili hususan wale wanaofanya vizuri, hivyo basi munapaswa kuongeza
juhudi ili kuwaunga mkono” alisema
Aidha, amewataka wanafunzi hao
kujiepusha na matumizi mabaya ya simu za mkononi na badala yake kuzitumia kwa
malengo mazuri ikiwemo kujifunza mambo mbali mbali yanayoendana malengo yao.
“Niwaombe sana juu matumizi ya simu hususan hizi smartphone, simu hizi zina mambo mengi sana mazuri na mabaya ni juu yako kuchagua unataka kuitumiaje, kwa hivyo nawaomba sana kwa wale wwnye simu kubwa kuzitimia vizuri simu hizi katika kujifunza mambo mbali mbali yanayoendana malengo yenu” Ali Juma Nassor
Kwa upande wake, Katibu wa jimbo la
Chambani Amour Kheri Vuai, amewasihi wanafunzi hao kutokujiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi kwani kufanya hivyo kupelekea kutokufanikiwa kimasomo pamoja
na kukatisha ndoto zao.
“Niwaahidi kuwa mwanafunzi yeyote
ambaye atajiingiza katika mambo ya mapenzi ni vigumu kufanya vizuri katika
masomo yake, kwasababu muda mwingi huutumia katika kufikiria mapenzi badala ya
masomo, kwa hivyo nawaomba sana kutokujihusisha na mapenzi nyinyi sasa hivi kazi
yenu ni moja tu ya kusoma basi” aliwasihi
Nae, mwalimu mkuu wa skuli ya msingi
Ngwachani Asha Haroun Abdalla, amewashukuru viongozi wa jimbo la Chambani kwa kujitoa
kwao kuisaidia sekta ya elimu katika jimbo na kuwaomba kuendelea na moyo huo ili
kukuza sekta ya elimu katika jimbo hilo.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya msingi Ngwachani, Asha Haroun Abdalla, akitoa neno la shukurani kwa Viongozi wa Jimbo la Chambani.
“Niwapongeze sana viongozi wetu wa
jimbo la Chambani kwakweli wanajitoa sana katika kuisaidia sekta ya elimu
katika jimbi hili, ni waombe waendelee na moyo huu huu ili kuhakikisha sekta ya
elimu katika jimbo hili inafanya vizuri” mwalimu mkuu
Nao, wanafunzi hao wameahidi kusoma
kwa bidii ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha
nne na sita.
Wanafunzi waliofaulu darasa la sita 2021 kutoka Skuli nne za Jimbo la Chambani.
Skuli hizo nne (4) ambazo
zimefanikiwa kufaulisha wanafunzi hao wa darasa la sita (6) mwaka 2021 ni Skuli
ya msingi Ngwachani ambayo imefaulisha wanafunzi kumi na nne (14) Skuli ya
msingi ukutini wanafunzi wawili (2) Skuli ya msingi Dodo wanafunzi (2) na Skuli
ya msingi Mizingani mwanafunzi mmoja (1) na kuifanya idadi ya wanafunzi kuwa
kumi na tisa (19).
Mwisho.