Wanakikundi Cha kuweka na kukopa cha Shehia ya Kilindi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kisanduku kilichokuwa wakihifadhia Fedha zao zenye thamani ya Shillingi milioni tatu na laki mbili kuchukuliwa.
Akizungumza na idawaonline.com muweka Hazina wa kikundi hicho aliyefahamika Kwa jina la Habiba Ziadi Ali, amesema alikuwa anaswali alishutuka baada ya kuhisi kisanduku kilichokuwa na fedha hizo kutokuwepo uvunguni Mwa kitanda ambako alikuwa anakihifadhi kisandugu hicho.
Bihawa Juma Rubea miongoni walioweka Fedha katika kikundi hicho ambaye alikuwa ameweka hisa ya shilingi laki mbili na elfu khamsini ambazo alipanga kuzifanyia shughuli mbali mbali ikiwemo biashara ndogo ndogo.
Nassor Mohammed Khamis ni Sheha wa Shehia ya Kilindi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa Wananchi wanaojishughulisha na vikundi vya kuweka Fedha na kukopa kuzihifadhi fedha banki pindi Fedha zao zinapokuwa nyingi ili kuepuka kuibiwa.
Nikiripiti kutoka Shehia ya Kilindi Mkoa wa Kusini Pemba Mimi ni