WAZAZI WATAKA MWALIMU AFUKUZWA SABABU YA UZURI WAKE UNAO WACHANGANYA WANAFUNZI

0

 

Mwalimu wa sanaa Kutoka New Jersey Nchini Marekani amejipata katika mzozo mkali na wazazi baada ya wazazi hao kuteta kutokana na umbo lake wakidai linawachachafya wanafunzi darasani.

Mwalimu huyo amekosolewa vikali kwa umbo lake alivyoumbika huku wazazi wakimtuhumu kuwa msumbufu wa akili za wanao.

Umbo lake na mavazi yake ni sababu kubwa kuwa inawafanya mpaka watoto wabaki kumuangalia mwalimu badala ya kupata kile anachokifundisha Darasani, Wazazi walisema umbo lake na muonekano wake ni tatizo kwa watoto wao.

Mwalimu huyo ni maarufu sana kwenye Instagram ambapo yeye hupakia mara kwa mara picha zake akiwa darasani na pia akifanya shughuli nyingine za kufurahisha akiwa nje ya shule.

Baadhi ya wazazi wanadai afukuzwe kazi huku wengine wakisema avae tu nguo zinazoficha maumbile yake.

Chini ya sheria ya New Jersey na sheria ya shirikisho la kazi, itakuwa kinyume cha sheria kwa shule kumfukuza kazi mwalimu kulingana na sura yake, ambayo labda ndiyo sababu na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya malalamiko yanayodaiwa ambayo yametolewa kuhusiana na sura ya mwanamke huyo na umbile lake.

Taarifa hiyo ilichapushwa na majarida na wanablogu wengi kote duniani huku wengi wakivutiwa na umbo la mwalimu huyo na kusema kwamba haina haja ya wazazi kuteta kwani wanafunzi anaowahudumia bado ni wadogo kufikiria mpaka kiwango cha mapenzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top