Wazazi Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kuwadhibiti watoto wao kutokushiriki uchumaji wa zao la karafuu ili waweze kuendelea na masomo yao na kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji.
Akizungumza na na masheha
pamoja na wakulima wa zao la karafuu katika ukumbi wa makonyo Wawi na ZSTC Mkoani Mkuu wa Mkoa wa Kusinie
Pemba Mhe. Matar Zahor Massoud, amesema wakati wa mavuno ya karafuu kuna
jitokeza vitendo vingi vya udhalilishaji
wa kijinsia kwa watoto, hivyo ni
vyema kwa jamii kuweka utaratibu wa
kuwahamasisha watoto kuhudhuria masomo.
Akizungumzia sheria na kanuni
za karafuu katibu wa shirika la
biashara la taifa ZSTC Ali Hilal Vuai, amesema shirika hilo halina wakala wa ununuzi wa karafuu na atakaebainika kufanya biashara hiyo pamoja na kutumia nembo
ya shirika la ZSTC hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Wakulima wa zao la karafuu, wachumaji, waokota mpeta (karafuu zinazoanguka chini) pamoja na wafanya biashara visiwani Zanzibar wanajiandaa kufaidika na zao hilo kwa msimu wa mwaka.
Zao la karafuu huchumwa kwa mwaka mara mbili kupitia msimu wa Vuli na mwaka.
Habari na, Zbc radio.
KAMA HUKUTAZAMA VIDEO HII YA MWENYEKITI WA CCM KUTAKA WANAUME WAOE WANAWAKE WENGI BOFYA SASA