WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA MPANGO WA UTETEZI WA HAKI ZA WANAWAKE KUHUSU UENDELEVU WA HAKI ZA KIJAMII.

0

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, amezindua Mpango wa Utetezi wa haki za Wanawake kuhusu uendelevu wa haki za kijamii. Uzinduzi huo umefanyiak JijiniDar es Salaam  tarehe 18 Agosti, 2022.

Waziri Dkt Doroth Gwajima

Katika hotuba yake Dkt. Gwajima amesema kuwa mpango huu unatoa namna iliyobora ya kushughulikia changamoto za kijinsia kwa nyakati za sasa.

Amesema Mpango huo ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuweka mikakati ya kuhakikisha tunashughulikia vyema changamoto za janga la UVIKO-19 na kudhibiti majanga mengine yanayoendelea kwa kuweka mbele maslahi ya wanawake na wasichana.
 

"Hii ni kwa sababu wanawake na wasichana wanapata athari kubwa kutokana na majanga haya, kwa hivyo tunahitaji kutambua na kushughulikia mahitaji yao ipasavyo." Dkt. Gwajima

Aidha, mpango huo umejikita kushughulikia masuala muhimu katika sekta ya matunzo, ulinzi wa kijamii, kuimarisha maisha ya wanawake, na hatua za utetezi wa haki za wanawake kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi.

Uzinduzi huu pia unalenga kuunda jukwaa la majadiliano nia ikiwa kuleta mitazamo chanya ya kuhakikisha kuwa tuna Sera, Mipango na Mikakati, inayozingatia jinsia ili kuwapatia maisha endelevu na ustahimilivu wanawake dhidi ya majanga yanayoweza kujitokeza.

Utekelezaji wa mpango huu unaenda sambamba na ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutetea haki za kiuchumi kwa Wanawake aliyotoa kwenye Kongamano la Kimataifa lililofanyika nchini Ufaransa.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Zainab Chaula alisema katika wakati wa sasa kunahaja yakuwa na Mfuko wa pamoja wa masuala ya jenda.

Tukio hili limehudhuriwa na wadau mbalimbali wanaoshirikiana na serikali katika uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya jinsia Mhe. Pamela Odonel Balozi wa Canada nchini Tanzania na Bi Hodan Odou Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchini Tanzania,
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top