ZAPA- YATOA MAFUNZO YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA WANANCHI 65 KUTOKA SHEHIA 6 ZA WILAYA YA MKOANI.

Hassan Msellem
0

Wahitimu wa mafunzo ya uraia na demokrasia wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo waliyopatiwa pamoja na kuyatoa kwa wananchi wengine ili waweze kutambua haki na wajibu wao katika Jamii na taifa kwa ujumla.Mapema akifunga mafunzo hayo ya siku mbili yaliyohusu elimu ya Uraia na demokrasia, yaliyoandaliwa na jumuiya ya kupambana na umaskini Zanzibar 'ZAPA', afisa utumishi kutoka ofisi ya mrajis wa jumuiya zisizo za kiserikali Pemba, Saada Abuubakar Khamis, Alisema elimu ya raia ndio elimu pekee inayoweza kuwaweza wananchi kuweza kutambua haki na wajibu wao katika taifa, hivyo basi amewaomba wahitimu hao kuyatumia mafunzo hayo ili iweze kuleta tija kwao na Jamii Kwa ujumla.


Aliongeza kuwa, elimu ya uraia inaweza kuwawezesha wananchi kutambua nafasi zao katika ujenzi wa taifa pamoja na kushiriki shughuli mbali mbali za kitaifa ikiwemo kupiga kura ili kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo katika taifa.


“Kuna umuhimu mkubwa sana kwa wananchi kuifahamu ya elimu ya uraia kwasababu inamuweza mwananchi kuweza kufahamu haki na wajibu katika taifa pamoja na kushiriki katika shughuli mbali za kitaifa ikiwemo kushiriki katika zoezi la sense, kupiga kura na kadhalika” alisema


Afisa utumishi kutoka ofisi ya mrajis wa jumuiya zisizo za kiserikali Pemba Saada Abuubakar Khamis akifungua Mafunzo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi kutoka 'ZAPA' Mohammed Said Ali, alisema mafunzo hayo yatawapa mwanga nzuri wananchi hao katika kufahamu elimu ya uraia pamoja na demokrasia.


Mkurugenzi wa jumuiya ya jumuiya ya kupambana na umaskini Zanzibar 'ZAPA' Mohammed Said Ali, akimkaribisha mgeni Rasmi.

“Ni matumaini yangu kwamba mafunzo haya yatawasaidia sana kwani mutaweza kujifunza mambo mbali mbali kuhusu elimu ya uraia, umuhimu wa demokrasia pamoja na utatuzi wa migogoro katika jamii zenu kwa njia ya amani na utulivu” alisema


Akiwasilisha mada juu ya elimu ya Uraia na Demokrasia msaidizi wa Sheria Wilaya ya Mkoani Suleiman Salim Mohammed, alisema miongoni mwa faida za demokrasia katika jamii ni wanajamii kushirikishana katika mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya ndoa, jambo ambalo hupunguza migogoro na vurugu ambazo hujitokeza mara kwa mara.

 

Aidha alisema, endapo suala la demokrasia litatekelezwa kwa vitendo kutapunguza malalamiko mbali mbali ambayo hujitokeza katika jamii kwani mwananchi atapata haki na fursa sawa bila ya kujali, rangi, dini wala kabila.


Msaidizi wa Sheria Wilaya ya Mkoani Suleiman Salim Mohammed akiwasilisha mada ya uraia na demokrasia.


Alisema “Kwakweli kuna faida nyingi za demokrasia katika ngazi ya kijamii na hata kitaifa lakini moja miongoni mwa faida hizo ni wanajamii kushirikishana katika mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya ndoa”


Evelyn Mchau ni Afisa programu kutoka taasisi ya Foundation For Civil Society 'FCS', amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri katika jamii ili mafunzo hayo yaweze kuleta tija kwao na taifa kwa ujumla.


Akitoa neno la shukurani  kwa niaba ya wahitimu wenzake, Ali Khamis Juma, ameushukuru uongozi wa ZAPA pamoja na taasisi ya Foundation For Civil Society kwa kuandaa Mafunzo hayo yenye faida kubwa wananchi.


Nao washiriki hao, ameahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo pamoja na kuyatoa kwa wananchi wengine ili jamii iweze kutambua haki na wajibu wao katika Ujenzi wa Taifa.


Mafunzo hayo ya siku mbili na yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya elimu ya Uraia pamoja utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani yamejumuisha wananchi 65 kutoka shehia 6 za Wilaya ya Mkaoni ambazo ni sheia ya Mgagadu, Mngwachani, Mbuguani, Dodo na Wambaa, ambayo ymeandaliwa na jumiya ya Zanzibar Anti-Povery Association 'ZAPA' chini ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society 'FCS'.


Mwisho.

 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top