HAROUB ATUHUMIWA KUMVAMIA BINTI SHAMBANI NA KUMBAKA .

Hassan Msellem
0

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20, mkaazi wa kijiji cha Mtendeni Jambangome Shehia ya Mizingani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba jina limehifadhiwa, amelazwa katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kutokana na maumivu makali aliyoyapata baada ya kubakwa wakati akiokota MPETA karafuu zinazodondoka chini” na kijana aliefahamika kwa jina la Abdillahi Haroub Suleiman mwenye umri wa miaka 20, mkaazi wa Kijichi Shehia ya kiuyu Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba na kisha kutoroka kusikojuilikana.

Pich kutoka Maktaba haihusiani naa tukio halisi

Akizungumza na idawaonline.com, mama mzazi wa mwanamke huyo aliebakwa, amesema tarehe 27, Agosti mwaka 2022 majira ya saa 11 za jioni alipokea ujumbe mfupi wa simu ‘sms’ kutoka kwa mtoto wake huyo uliomtaka kufika eneo husika ambalo ulionesha mtoto wake huyo akiwa katika mazingira ya maumivuy makali na kusema anakufa ndipo haraka kwa kushirikiana na majirani kumtafuta mwanamke huyo hadi kufanikiwa kumuona.


“Alitoka na wenzake kwenda kuokota MPETA wakati anarudi ndugu zake walibaki mikarafuu wakiwa wanaendelea kuokota MPETA na kufuatana na mwenzake ambaye walikuwa wanachanganya zile karafuu, akamuambia jana sijachukua kuni kwahivyo leo nataka nichukue kuni, ndipo alipotokea kijana ambaye alimuuliza unaenda wapi akamjibu natafuta kuni hapo hapo akamkamata na kumtia kanga ya mdomo akamchukua akampandisha juu milimani na kwenda kumfanyia hicho kitendo” alisema mama hayo.


Fatma Mohammed Juma ni Sheha wa shehia ya Mizingani, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi hususan akina mama na wasichana kuachana na tabia ya kwenda kuokota mpeta na kuni katika kipindi hichi cha uchumaji wa zao la karafuu wakiwa peke yao na badala yake kwenda makundi makundi ili kuepukana na vitendo vya udhalilishaji vinavyoweza kujitokeza.

SOMA HII /JIFUNZE NAMNA YA KUPATA TSH 1000 BURE KUPITIA TIGO PESA au M PESA

“Nakiri kutokea kwa kitendo cha ubakaji kwa kijana nayeitwa Abdillahi Haroub Suleiman mwenye umri wa miaka 20, mkaazi wa Kijichi Kiuyu Wilaya ya Micheweni kumbaka msichana wa miaka 20 jina nalihifadhi, nitowe wito kwa wananchi hususan akina mama na wasichana waachane na tabia ya kwenda kuokota MPETA wakiwa mmoja mmoja na badala yake kwenda kwa makundi makundi ili kuepukana na vitendo vya udhalilishaji vinavyoweza kujitokeza kwa mfano kama huyu binti aliebakwa kama angalikuwa na wenzake mwanzo hadi mwsiho nadhani asingalifanyiwa unyama huo” alisema

Kwa upande wake, kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Daktari Said Ismail Ali, amethibitisha kupokewa kwa mwanamke huyo Agosti 27, 2022 majira ya saa 12:30 za jioni walimpokea mwanamke mwenye umri wa miaka 20, baada ya kufanyiwa kitendo cha udhalilishaji ambapo alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa amebakwa na kuendelea na matibabu zaidi.

“Jana tarehe 27 majira ya saa 12:30 za jioni tulimpokea muathirika ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 aliletwa hospitali inasemekana kuwa  alibakwa akachunguzwa ikathibitika kweli kafanyiwa kitedno cha ubakaji, kwahivyo bado yupo hospitali kalazwa na anaendelea na matibabu zaidi” Kaimu mganga mkuu hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani

Ikumbukwe kuwa katika misimu ya uchumaji wa zao la karafuu vitendo vya udhalilishaji hutajwa sana kushamiri katika maeneo mbali mbali kisiwani Pemba, hivyo basi tunawaomba wananchi hususan wanaume kuendelea na harakati za uchumaji wa zao la karafuu bila ya kuathiri utu wa akina mama na wasichana, pamoja akina mama na wasichana nao kutokuchangia vitendo hivyo kwa namna moja ama nyengine.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top