AHUKUMIWA VIBOKO 6 KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 13

0

 Kijana John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati Mkoani Manyara amehukumiwa kuchapwa viboko sita baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka kumi na tatu (13) aliyekuwa anasoma darasa la nne ambapo kijana huyo alitekeleza tendo hilo Septemba 10, 2021

Picha haihusiani na mtuhumiwa aliyehukumiwa -kutoka Maktaba

Hukumu hiyo imetolewa hii leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara chini ya Hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo Mariamu Rusewa na wakili wa serikali Petro Ngassa, ambapo ameiambia mahakama kwamba kosa hilo la ubakaji ni kinyume na vifungu vya mia moja na thelathini kifungu kidogo cha kwanza na kifungu kidogo cha pili (e), kifungu cha mia moja thelathini na moja (2), (a) kifungu kidogo cha kanuni ya adhabu sura namba kumi na sita kama ilivyofanyiwa marejeo toleo la mwaka 2019.

Sheria hiyo inaeleza kama mvulana wenye umri wa miaka kumi na nane au chini ya miaka hiyo na kwamba ikiwa ni kosa lake la kwanza hukumu yake ni kuchapwa viboko.

Kabla ya hukumu hiyo kutekelezwa kijana huyo John Emmanuel atapelekwa hospitali kupimwa kama ni mzima wa afya ndipo atakapochapwa viboko hivyo sita
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top