Mwanadada wa Nigeria kwa jina la Olaitan ameripotiwa kujiua baada ya mwanaume aliyekuwa nae katika mahusiano kuchukua pesa zake ili kwenda kuoa mwanamke mwingine kupitia pesa za mrembo huyo
Mwanadada huyo alikuwa anaweka pesa zake katika akaunti ya jamaa husika ambaye hakuwa na kazi ya kueleweka kwani mdada ndie alikuwa ameajiriwa na kumpa jamaa hata pesa ya matumizi ya hapa na pale
Alhamisi wiki iliyopita walikuwa pamoja na hata usiku wa kuamkia ijumaa walikuwa pamoja na huyo mwanaume kwa jina la Saheed.
Baadaye rafiki akamtonya mdada kuwa jamaa anaoa wikiend ambapo mdada alipatwa na mshituko na baada ya kuangalia pesa katika akaunti ya jamaa akakuta hakuna kitu zote zimekombwa na jamaa
Mdada huyo ameelezwa kunywa kitu chenye sumu iliyopeleka kifo chake hivyo kuacha mtoto wake mwenye miaka 7.