Mahakama maalumu ya makosa ya Udhalilishaji Chake Chake jana September 22.2022 imempeleka rumande Massoud Khamis Mussa mwenye umri wa miaka 23 Mkaazi wa Vikunguni wa tuhuma za kumdhalilisha kingono mtoto wa kiume wa miaka tisa (9).
Ilielezwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Asia Ibrahim Mohammed, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye Nyengo, kwamba mnamo tarehe 14.09.2022 majira ya saa 09:00 za jioni huko Vikunguni Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba mshitakiwa alimdhalilisha kingono mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa (9) jina linahifadhiwa jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mshitakiwa baada ya kusomewa shitaka lake
alikana, ndipo hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye Nyengo alipomuamuru
Mshitakiwa kwenda rumande hadi tarehe Octoba 03.2022 kesi itakapoanza
kusikilizwa ushahidi.