JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Katekista Athanas Lugambwa (62) mkazi wa Mganza wilayani Chato mkoani Geita kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Katema.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe, amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu ya kumvizia mtoto huyo anapokwenda kusoma mafundisho ya Dini Kanisani na kumuita ofisini kisha kumbaka.
Kamanda Mwaibambe amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.