ATUHUMIWA KUMUUA MAMA YAKE KWA KUMYIMA CHAKULA MJUKUU WAKE.

0

Elisha Mwena (42) mkazi wa Kijiji cha Idofi kilichopo katika halmashauri ya mji wa makambako mkoani Njombe ambaye ni mlemavu wa macho anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kosa la kumpiga na kumsababishia umauti mama yake mzazi Elina Nzilano (87) kwa sababu ya kumnyima mtoto wake chakula.


Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mama huyo alimnyima chakula mjukuu wake kwakuwa aliiba kuku na kumla peke yake ndipo bibi yake huyo akaamua amuadhibu kwa kumnyima chakula.

Kamanda Issa amesema kitendo hicho kilimkasirisha baba wa mtoto huyo ambaye ni mlemavu wa macho ndipo akachukua fimbo yake na kumpiga mama yake huyo na kumuumiza na alipopelekwa hospitali alifariki.

Katika tukio lingine Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia watu 11 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya mlinzi wa mradi wa ujenzi wa chuo cha veta kinachojengwa wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top