ATUPWA JELA KWA UBAKAJI WA MWANAE

0Mwanaume mmoja aliefahamika kwa jina la Charles Rebei mwenye umri wa miaka 52 mkazi wa Kiteto mkoani Manyara amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mwanae wa miaka saba.


Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo mshitakiwa alikumbushwa kosa lake na mwendesha mashtaka wa serikali mkaguzi wa Polisi Wilfred Mollel kuwa huko katika kijiji cha Kimana Kata ya Batibo wilayani Kiteto mkoani Manyara kwamba Septemba 23, 2021 alimbaka mwanae.


Mshtakiwa alikana shitaka lake kwa mara ya kwanza baada ya kusomewa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kiteto na alidai kuwa hana mashahidi huku upande wa mashtaka ukiwa na mashahidi watano.


Kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hakimu amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kubaka na kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa alipewa ruhusa ya kuiomba mahakama ili iweze kumpunguzia adhabu ambapo amemuomba hakimu kumpunguzia adhabu kwani yeye ni mzee.


Aidha kwa upande wa mashtaka umeiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani vitendo vya ubakaji wilayani Kiteto vimekithiri ili iwe fundisho kwa watu wengine hivyo hakimu alisoma hukumu hiyo akimtia hatiani kwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top