AUAWA BAADA YA KUMKUMBATIA MKE WA MTU

0

Mtu anayefahamika kwa jina la Razalius Kufabasi (50) mkazi wa kijiji cha Lusala wilayani Ludewa mkoani Njombe anashikiliwa na jeshi la polisi  kwa kumpiga na tofali la kuchoma Linus Mtega (52) na kumsababishia umauti.

Imeelezwa kuwa siku ya tukio hilo kulikuwa na shughuli ya kujengea makaburi ambapo majira ya usiku watu walikuwa wakiburudika kwa muziki hivyo marehemu huyo alikuwa amemkumbatia mke wa mzee Kufabasi huku wakicheza pamoja kitu ambacho kilimpa wivu mzee huyo na kupelekea kuchukua tofali na kumpiga nalo mzee Mtega kwenye paji la uso.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mzee Mtega alichanika paji lake la uso ambapo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Mlangali lakini hakuweza kupona na kufikwa na umauti huku  mtuhumiwa huyo akijaribu kutoroka lakini hakuweza kufanikiwa na kutiwa nguvuni na jeshi la polisi.


Kamanda Issa amelaani vikali tabia hizo huku akiitaka jamii kuacha wivu uliopitiliza kwani yanapotokea mauaji kama haya familia pamoja na watoto ndio huteseka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top