Waliokuwa watumishi wanne (4) katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete wamefukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha za Mapato ya ndani na mmoja ni utoro kazini na kuisababishia hasara Serikali.
Maamuzi hayo ni
kufuatia Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani lilikutana leo kujadili maadili
ya watumishi zaidi ya 60 ambapo kati ya hao watumishi wanne wamefutwa kazi na
watumishi watano (5) wameagizwa kukatwa mishahara yao 15% kwa mwaka mmoja,
wengine miaka miwili na mmoja miaka mitatu
Watumishi waliofukuzwa
kazi ni aliyekuwa Mtendaji Kata ya Mbalatse Omega Aloyce Thobias ambaye
amefukuzwa kwa utoro kazini kwa kipindi cha siku 214.
Watumishi wengine ni
waliokuwa watendaji wa vijiji ambao ni Bryson Isaack Sanga aliyekuwa Mtendaji
wa Kijiji cha Ludihani, Godwin Jacob Luvanda aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha
Ikuwo na Tumaini Shem Ngogo aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kigala
Watendaji hao watatu
wamefukuzwa kwa ubadhirifu wa fedha za mapato ya ndani ambapo Tumaini Ngogo
amekusanya fedha zaidi ya Milioni 44 na kupeleka Bank.
Akizungumza na
waandishi wa Habari baada ya Kikao hicho, Mkueugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Makete William M. Makufwe amesema kufuatia kubainika na makosa
watumishi hao wamefutwa kazi kuanzia sasa.
“Niwasihi watumishi
wengine tuliopo kazini zama za kutumia fedha za makusanyo zikiwa chini ya
makusanyo yao zimeshapitwa na wakati na unakamatwa wakati wowote…ukikusanya
kuanzia shilingi laki tano hakikisha fedha hizo zinakuwa salama kwa kupeleka
Bank ili waepuke kingia kwenye vishawishi vya wizi wa fedha hizo”.
“Kuhusu huyu Mtumishi
ambaye amekuwa mtoro kwa kipindi cha zaidi ya siku 200 naye amefukuzwa kazi kwa
kutokuwepo kazini wakati taratibu zote za kumfuta kazi zimefanyika kwa kufuata
sheria za utumishi”
Kwa niaba ya Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri (W), Diwani Kata ya Mfumbi Mhe. Atilyo Ng’ondya
amesema watumishi wanapaswa kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali kwa
kuwa Serikali ina mkono mrefu na vyombo vingi katika kuwasimamia watumishi
wake.