Familia ya kijana Fahad Mohammed, miaka 13 mkaazi wa Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, anayesoma darasa la nne mwenye ulemavu wa viungo wameshusha punzi ya faraja baada ya kujengewa choo cha kisasa kutokana na changamoto ya ukosefu wa choo iliyokuwa ikimkabili mtoto wao mwenye ulemavu wa viungo kwa muda mrefu hali iliyomlazimu kijana huyo kujisaidia porini, hali ambayo ilikuwa ni hatarishi kwa afya yake.
"Kunradhi ndugu msomaji kwa kuona picha ambayo mwandishi wa habari hii hakufahamu kuwa kutumia picha ya mtoto huyo akiwa kwenye choo bila ya kuwa katika mazingira salama ikiwemo kutokuvaa viatu vya mikono wala miguu"ameandika mhariri
Akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa wilaya ya Mkoani Pemba, Mheshimiwa Khatib Juma MjajA, Mama mzazi wa kijana huyo Asha Mnahaki Faki, amesema wamejisikia faraja kubwa kwa kupatiwa msaada huo wa kujengewa choo kwani hali ya mtoto wao huyo mwenye ulemnavu wa viungo ilikuwa ni mbaya kutokana na kunisaidia katika mazingira hatarishi ikiwemo vichakani.
"Kwakweli tumefarijika sana sana kwa kujengewa choo hichi kwasababu tulikuwa hatujui tufanyeje na sisi ni maskini hatuna uwezo hata wa chakula seuze kujenga choo cha kisasa lakini tunashukuru kwasababu sasa mwenetu amepata sehemu sahihi ya kujisaidia' alisema mama wa mtoto huyo
![]() |
Mama mzazi wa kijana mwenye ulemavu wa viungo Bi. Asha Mnahaki Faki, kitoa neno la shukurani kwa kupatiwa msaada wa kujengewa choo na sabuni. |
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mheshimiwa Khatib Juma Mjaja, ametoatoa ahadi ya kumsaidia godoro Kijana huyo ili awe na Mazingira safi na salama ya kupunzisha mwili baada ya harakati za siku mzima.
"Binafsi nimeguswa sana na Mtoto wetu huyu na niwaahidi kuwa nanyi bega Kwa bega Kwa msaada wowote mutakaohitaji na naahidi kutoa msaada wa godoro litakalomsaidia kupata mazingira safi na salama ya kupunzisha mwili" DC Mjaja

Aidha, Mheshimiwa Mjaja ametoa rai ya kujengwa kwa miundombinu mizuri ya kuweza kumsaidia kijana huyo kutoka na kuingia nyumbani kwao sambamba na kupatiwa vifaa mbali mbali ikiwemo kitimwendo kitakachomsaidia kwenda katika shughuli zake.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Mjaja alitoa msaada wa Pempasi na Sabuni kwa kijana huyo ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Mkoani.
Nae, Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, amewashukuru wanajamii pamoja na pamoja na Bi. Asia Abdallah Omar, mwalimu wa Skuli ya msingi Ngombeni B ambaye aliwahamasisha wanajamii waliomzunguka kijana huyo pamoja na majirani wanaoishi Ulaya kuchangia ujenzi huo wa choo na kusema kitendo hicho ni chema na kinapaswa kuigwa na Jamii nyengine zenye watu wenye mahitaji mbali mbali.
"Kwakweli nimefuruhishwa sana na hili napia nitoa shukurani na pongezi zangu Kwa wanajamii wote pamoja na muhisanani ambaye kwa moyo dhati alijitoa moyo mmoja kulisimamia hili Hadi kufikia ukingoni hatimae leo kijana wetu anapata sehemu nzuri ya kujisaidia, niseme tu kuwa duniani Mungu atamlipa lakini Akhera atalipwa ujira mkubwa zaidi" Bi. Warda
Akielezea gharama zilizotumika katika Ujenzi was choo hicho, mwalimu wa Skuli ya msingi Ng'ombeni Bi. Asia Abdallah Omar, amesema choo hicho kimegharimu shilingi Zakitanzania milioni moja laki tano kwenye shilingi millioni Moja na laki nane zilizochangwa ambapo shilingi laki tatu zilizobaki zimenunuliwa matofali ya hakiba pindi ikitokea dharura.
Ikumbukwe kuwa, September 11.2021 idawaonline.com kwa kushirikishana na afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed, ilimtembelea kijana huyo na kuzungumza na wazazi juu ya changamoto hiyo inayowakabili Mtoto wao huyo mwenye ulemavu wa viungo.
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=pfbid02ftHHrKqaS2WeXsPRta6UEtJLi75qGrostFDDVKV3ntqCnCRdbGnapC7cwsx3fzAjl&id=100015016364837.
Hapo juu ni kiungo (link) cha habari ya Facebook ambayo niliandika baadaya kunitembelea familia ya Mtoto huyo mwenye ulemavu wa viungo wakati wakihitaji msaada wa kujengwa choo.
Picha ya kijana Fahad Mohammed Ame, mwaka September 10.2021 alipotembelewa na Afisa wa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Waly Mohammed na Mwandishi wa Habari wa Idawaonline.com
Kupatikana kwa msaada huo wa ni ushirikiano na utakelezaji wa majukumu wa afisi ya Wilaya ya Mkoani kupitia afisa wake wa watu wenye ulemavu Warda Waly Mohammed kwa kushirikishana na waandishi wa Habari mbali mbali Kisiwani Pemba.