UKATILI; AHUKUMIWA MIAKA 50 CHUO CHA MAFUNZO KWA KUBAKA NA KULAWITI MTOTO

Hassan Msellem
0
Picha kutoka Maktaba.

Mshitakiwa Suleiman Haji Hamad mwenye umri wa miaka 29, mkaazi wa Mpendae amehukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka (50) kwa makosa matatu ya udhalilishaji aliyoyafanya kwa msichana mwenye umri wa miaka kumi na nne (14).

Hukumu hiyo ilitolewa 02 Septemba mwaka 2022 na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga Omar Mcha.


Hukumu hiyo ya kutumikia miaka 50 chuo cha mafunzo imetokana hukumu ya miaka ishirini (20) kwa kosa la kutorosha, miaka kumi (10) kosa la kubaka miaka ishirini (20) na kosa kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo na miaka ishirini (20) lakini kwa vile adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja mwanafunzi Suleiman atatumikia miaka hiyo.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali Huda Othman, kwamba mshitakiwa Suleiman Agosti, 2019 majira ya saa 5 asubuhi alimtorosha msichana mwenye umri wa miaka 14, kutoka nyumbani kwao na kumpeleka nyumbani alipokuwa akiishi mshitakiwa huko Migombani Ngazimia na baadae baina ya saa 6 za mchana alitenda kosa la pili la kumbaka  na tena kufanya kosa la tatu la kumuingilia kinyume na maumbile.

Kesi hiyo ilifunguliwa January 01, 2022 na kuanza kusikilizwa January 14, 2022 ambapo idadi ya mashahidi saba upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi na baada ya hakimu Omar Mcha kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mlalamikaji na kutoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Hata hivyo mshitakiwa huyo atatumikia chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka ishirini (20) kwa vile kosa la kutorosha

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top