JELA MAISHA KWA KULAWITI MTOTO WA MIAKA 6

0

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa, imemuhukumu kifungo cha maisha, Ayubu Kiyanza (22) mkazi wa eneo la Don Bosco Manispaa ya Iringa, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka sita.

Alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2021, baada ya kumvizia mtoto huyo akiwa anatoka shuleni, kisha kumvutia kichakani huku akiwa amemziba mdomo, ili asipige kelele.

Baada ya kufika nyumbani baba yake alimuona mwanae akiwa mchafu tofauti na alivyomzoea na ndipo akamuhoji na mtoto huyo kumueleza kilichotokea.

Baada ya kumsikiliza, baba alimwambia mwanae ampeleke eneo alilofanyiwa ukatili na wakiwa njiani, walimuona mtuhumiwa huyo na ndipo taratibu za kumkamata zikafanyika.

Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2021 ilikuwa na mashahidi watano, akiwemo daktari aliyethibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa amelawitiwa.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Rehema Mayagilo, alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo haukuwa na shaka ya kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Ili iwe fundisho kwa watu wengine, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Veneranda Masai, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo kwa kuwa kitendo alichokifanya kimemuathiri sana mtoto huyo.

Alipopewa nafasi ya kujitetea, mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa madai kwamba ana mtoto mdogo na anamtegemea, ombi lililokatiliwa na mahakama hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top